
Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tabora Agrrey Mwanri na kulia ni Generro Gatusso.
Akiongea hivi karibuni kwenye moja ya mikutano yake ya ziara mkoani Tabora, Mkuu huyo wa mkoa aliahidi kuwa ataboresha michezo mkoani humo kwani yeye ni mtaalam wa soka kama wanasoka wakongwe.
''Unajua watu wanadhani mimi sijui michezo lakini mimi nilikuwa napiga chenga mpaka naukalia mpira na nilikuwa nafunga kama Gatusso tena kwa mguu wa kushoto na nikikaa golini nakuwa kama Emmanuel Okala au Mambosasa'', alisema Mwanri.
Emmanuel Okala ni mlinda mlango wa zamani wa Enugu Rangers na timu ya Taifa ya Nigeria ambaye alicheza kwa kiwango kikubwa miaka ya 1972 na 1980.
Mkuu huyo wa mkoa amewataja wachezaji wengine ambao anafafana nao viwango kuwa ni golikipa wa zamani wa Tanzania Athuman Mambosasa pamoja na Gennaro Gattuso beki wa zamani wa AC Milan na Italia ambaye kwasasa ni kocha wa AC Milan.