Mabondia Francis Miyeyusho chichi mawe wa kinondoni na Mohamed Rashid Matumla wa keko wanataraji kupambana april 26 mwaka huu jijini Dar es salaam katika pambano la kulipwa la uzito super Bantam kilo 55
Mpambano huo umetangazwa hii leo katika ukumbi wa vijana kinondoni jijini Dar es salaam ambapo mabondia hao pia walisaini mkataba wa pambano hilo ambao unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa masumbi hapa nchini
Mpambano huo utasimamiwa na organization ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBO chini ya Rais wake Yasin Abdalah Ustaadh ambaye amempongeza mratibu wa pambano hilo kwa kuwasainisha mkataba mabondia hao tendo lililofanyika kwa uwazi mbele ya waandhishi wa habari
Kwaupande wao mabondia hao ambao watakutana kwa mara ya kwanza siku hiyo baada ya kutafutana kwa muda mrefu kila mmoja ametamba na kujinasibu kumchakaza mwenzake siku hiyo
Ambapo wa kwanza alikua Francis Miyeyusho ‘chichi mawe’ ambaye ametamba kuendeleza kichapo kwa bondia huyo akimkumbusha kile alichokifanya kwa baba yake mdogo Mbwana Matumla Huku kwa upande wake bondia Mohamed Rashid Matumla 'snake junior' yeye akijinasibu kulipa kisasi kwa bondia huyo japo pambano hilo akikili kuwa litakua gumu mno.
