Tuesday , 1st Jul , 2014

Michuano ya Riadha taifa yanataraji kuanza kutimua vumbi July 12 mwaka huu katika uwanja wa Taifa DSM ikishirikisha mikoa zaidi ya 10 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Baadhi ya wanariadha katika mashindano ya Riadha Taifa yaliyowahi kufanyika katika uwanja wa Taifa DSM

Zaidi ya Mikoa 10 ya Tanzania Bara na Visiwani imethibitisha kushiriki mashindano ya Taifa ya Riadha yanayotarajiwa kufanyika Julai 12 mpaka 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Muhtasari wa Michezo leo, Mmoja wa wanakamati wa maandalizi ya mashindano hayo Thabit Bashir amesema mashindano hayo yanafanyika kwa lengo la kutafuta timu bora ya Riadha kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Thabit amesema mashindano haya yatasaidia kukuza vipaji vya vijana kwa kuwa baadaye itaundwa timu ambayo itaweza kushindana katika mashindano makubwa ya ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo Bashir amesema bado kuna changamoto ya waamuzi wa mchezo wa riadha na hivyo kabla ya kufanyika kwa mashindano hayo watalazimika kutoa mafunzo kwa waamuzi ili kuwe na usawa katika mashindano hayo