Wednesday , 20th Jul , 2016

Mashindano ya vijana kwa michezo mbali mbali ikiendelezwa, inaweza kuibua vipaji na kutoa fursa za kiuchumi. kutangaza utalii wa nchi, na kutoa ajira kwa vijana.

Sekta ya michezo nchini ikiendelezwa inaweza kutoa fursa mbali mbali za kiuchumu na kutangaza utalii wa nchi, ambao ni faida kwa kukuza uchumi.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa, Nape Nnauye amesema tayari, Watanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wametengeneza maisha yao kutokana na fursa waliyoipata kwenye mchezo wa soka, hivyo ana matumaini vipaji vingi vitaendelea kuvumbuliwa kupitia michezo.

Nape amepongeza juhudi zinazofanywa na baadhi ya makampuni, kama Aitel, na Coca Cola ambayo yana mashindano ya vijana kila, yanayojulikana kama Airtel Rising Stars, na Copa Coca Cola, ambayo yameibua vipaji vya vijana wengi, hivyo ametaka makampuni mengine yaige.