
Wachezaji wa Mchenga team (wenye jezi za njano) wakiminyana na Ukonga Warriors (jezi nyeupe).
Kutokana na ushindi huo, Mchenga team wataladhimika kusubiri matokeo ya jumla ambayo yatatolewa jioni ya leo baada ya mechi zote kuisha ili kujihakikishia kupata tiketi ya kuingia hatua ya nane bora katika michuano hiyo.
Pamoja na hayo, Mchenga team wameweza kutoa mfungaji bora Mohamed Yusuph kwa siku ya leo 'best scorer' kwa pointi 25 huku mpinzani wake Richard Rova akipata pointi 15 kutoka Ukonga Warriors.
Mohamed Yusup aliyeibuka kinara kwa kutupia vikapu 25 kutoka Mchenga team.
Richard Rova aliyetupia vikapu15 kutoka timu ya Ukonga Warriors
Mtanange huo wa kukata na shoka umechezeshwa na refa Edwin Kilagwa pamoja na msaidizi wake 'Empire' Faraja Jime