Sunday , 3rd May , 2015

Kama ilivyotegemewa na mashabiki wachache wa bondia Mayweather na pasipokutegemea kwa mashabiki wengi hii leo bondia mwenye rekodi bora katika ngumi za kulipwa uzito wa welter Floyd Money Mayweather ameweza kudhihirisha ubora wake katika masumbwi

Mayweather kushoto akimsukumia konde Pacquiao katika mpambano wao alfajili ya hii leo

Bondia asiyepigika raia wa Marekani Floyd Mayweather jr. amemaliza ubishi kwa kumtwanga Mfilipino Manny Pacquiao katika pambano lao lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa ulimwenguni kote.

Katika pambano hilo ambalo Pacquiao alikuwa akishangiliwa sana, ngumi zake nyingi zilionekana kuwavutia mashabiki, lakini ambazo hazikumpa pointi za kujenga ushindi

Mayweather  alikuwa makini zaidi na kuweza kupiga ngumi nyingi zenye pointi.

Miongoni mwa maelfu ya mashabiki waliohudhuria mpambano huo wa kihistoria ni familia ya bondia Mayweather jr
Huku miongoni mwa watu maarufu alikuwepo pia rafiki wa bondia huyo mwanamuziki Justin Biber

Na mwishoni huku Pacquiao akijaribu kutafuta Knock Out mwenziye alikuwa akimkwepa na kumkimbia na hadi mwisho wa mpambano huo Mayweather alitwaa mkanda wa dunia wa WBC baada ya kupata ushindi wa point kwa maamuzi ya majaji wote watatu [majority decisions] na wawili hao kukumbatiana kuonyesha mchezo ni si uadui.

Awali kabla ya mpambano huo mabondia hao walikua na rekodi tofauti ambapo Pacquiao alikua amecheza mapambano 47 na kupoteza 5 akitoka sare mawili huku akishinda kwa knock out mapambano 37 na matatu kwa pointi

Huku kwa upande wake Mayweather yeye alikuwa amecheza mapambano 37 akishinda yote, 26 kwa Knockout na 11 akishinda kwa pointi.

Matokeo hayo yanamfanya Mayweather kuendelea kuwa bondia pekee asiyepigika katika uzito wa welter na anakuwa bondia ambaye anaingiza pesa nyingi katika mchezo huo kwa sasa kwani inasadikiwa katika mpambano huo wenye thamani ya zaidi ya paundi milioni 300 ukiondoa bonasi zingine Mayweather anataraji kujizolea kitita cha zaidi ya paundi milioni 180.