Friday , 18th Jul , 2014

Maximo asema anataka wachezaji kucheza kitimu badala ya kumtegemea mtu mmoja na amesisitiza kuwa hakuna mchezaji wa kipekee katika timu hiyo na ametaka usawa katika timu hiyo

Kocha mkuu wa timu ya Yanga Mbrazil Marcio Maximo.

Kocha mkuu wa timu ya soka ya Yanga ambayo inaendelea na mazoezi yake katika shule ya sekondari ya Loyola jijini Dar es salaam Mbrazil Marcio Maximo amesema hivi sasa anataka kuijenga timu hiyo icheze kitimu zaidi kuliko kucheza kwa kumtegemea mchezaji fulani kitu ambacho kinaathali pindi mchezaji husika anapokosekana

Maximo amesema amejifunza mengi hasa kupitia kombe la dunia nakuona jinsi gani timu zilizokua zikiwategemea baadhi ya wachezaji mmoja mmoja zilivyoathilika tofauti na zile ambazo zilicheza kitimu akitolea mfano mabingwa wa dunia timu ya taifa ya Ujerumani

Aidha Maximo ambaye anakinoa kikosi cha timu hiyo akisaidiwa na wasaidizi wake watatu Mbrazil mwenzake Leonaldo Leiva na Watanzania Salvatory Edward pamoja Juma Pondamali ambaye ni kocha wa makipa amesema hivi sasa anaingiza mfumo wa timu hiyo kucheza kitimu muda wote kama ilivyo kwa wajerumani kwa ambao walifuatilia mashindano ya kombe la dunia watakubaliana na kauli yake

Ambapo Maximo ametolea mfano timu za Brazil ambayo tangu ilipopata pengo la mshambuliaji wake Neymar aliyeumia basi ikapoteza mwelekeo kabisa huku pia kwa upande wa Argentina nao waliathilika na hali ya mshambuliaji wao tegemeo Lionel Messi kutokua katika kiwango chake katika baadhi ya mechi ama kutopata nafasi yakufanya vitu ambavyo huwa anavifanya akiwa na timu yake ya FC Barcelona ya Hispania baada ya kubanwa vilvyo na walinzi wa timu pinzani.

Maximo amesema ndio maana yeye ameligundua hilo mapema na sasa atahakikisha timu hiyo itakua ikicheza kwa mfumo wa kijerumani.