
Mohamed Matumla
Taasisi hiyo imesema bondia huyo atarejea katika hali yake ya kawaida katika kipindi cha miezi 08 hadi 12.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo Othmani Kiloloma amesema, mara baada ya kumpokea bondia Matumla walimfanyia uchunguzi wa kina na kugundua kuwa amepata athari katika ubongo hivyo wakalazimika kumfanyia upasuaji ili kuweza kuokoa maisha yake.
"Matumla aliletwa hapa Muhimbili saa nane usiku akiwa amepoteza kumbukumbu pamoja na fahamu na baada ya kumfanyia vipimo tuligundua kuwa amepata jeraha kichwani na kwenye ubongo ambalo limepelekea damu kuvilia kwenye ubongo kitaalam (Acute Subdyral Hemotoma) na kusababisha mgandamizo kwenye ubongo upande wa kulia ambapo alihitaji upasuaji wa haraka na wadharura," amesema Dokta Kiloloma.
Dkt Othman Kiloloma
Kiloloma amesema, upasuaji ulifanyika kwa mafanikio mwakubwa chini ya jopo la wataalam wazalendo watano kwa muda wa masaa matatu huku akiongeza kuwa mara baada ya upasuaji huo bondia huyo kwa sasa anaendelea vizuri na matababu.
Kwa upande wake Katibu wa Kamisheni ya mchezo wa ngumi za kulipwa Tanzania TPBC Chacha Michael amesema, Matumla alishindwa kuendelea na mpambano usio na ubingwa katika mzunguko wa saba lakini walifanikiwa kumuwahisha hospitali ambapo alifanyiwa upasuaji na sasa anaendelea na matibabu ili kuhakikisha anarudi katika hali yake ya kawaida.