Friday , 22nd May , 2015

Wanariadha watakaoshiriki michuano ya kimataifa ya mabingwa ya Pan African nchini Kenya wanatarajiwa kupatikana katika mashindano ya wazi ya Taifa yatakayofanyika kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika taarifa yake, Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini RT, Suleiman Nyambui amesema, mpaka sasa haijajulikana idadi ya wanariadha watakaokwenda Kenya kushiriki michuano hiyo ya Pan African itakayofanyika Mei 31 mwaka huu nchini humo.

Nyambui amesema, wanariadha watakaoonesha viwango vizuri katika mashindano ya wazi ya taifa hapo kesho ndiyo watakaochaguliwa kuunda timu ya Taifa itakayokwenda Kenya.

Nyambui amesema wanariadha na viongozi wote watakaoshiriki mashindano hayo ya wazi ya taifa wanatakiwa kujigharamia malazi, chakula na usafiri.