Monday , 27th Jun , 2016

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub Cannavaro amesema, anaamini timu wanayokutana nayo kesho ni kubwa lakini kila mchezaji amejiandaa kwa ajili ya kufanya vizuri katika mchezo huo.

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub Ally Cannavaro

Cannavaro amesema, anawaheshimu TP Mazembe na mchezo huo anauangalia kama fainali kwani ushindi wa kesho ndio utawaweka katika mazingira mazuri ya kuweza kusonga mbele.

Cannavaro amesema, anaamini kila mchezaji amejiandaa kwa ajili ya kuweza kuipa timu ushindi na kuweza kusonga mbele katika mshindano hayo.

Cannavaro amewataka mashabiki kufika kwa wingi kwa ajili ya kuweza kuwapa sapoti kwani pia wanachangia asilimia kubwa ya ushindi michezo mbalimbali.