Tuesday , 17th Feb , 2015

Mashabiki wa Soka hapa nchini wametakiwa kuwa na uzalendo kwa kuzipa sapoti timu zilizo ndani ya nchi yao.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa Habari wa Shirikisho la soka nchini TFF, Baraka Kizuguto amesema, iwapo timu pinzani inacheza na timu kutoka nje haina haja ya kushabikia timu kutoka nje isipokuwa unatakiwa kuipa sapoti timu yako ambapo ni ya nchi yako ili kuweza kuitangaza nchi.

Kizuguto amesema, mfumo wa ukataji tiketi pamoja na maeneo ya kukaa Mashabiki ndivyo vinavyochangia mashabiki hao kushindwa kuwa na umoja wa kuipa sapoti timu yake hivyo kupelekea wazawa kudharaulika na wageni.