Tuesday , 8th Sep , 2015

Shirikisho la Soka nchini TFF na vyama vimetakiwa kuwa na kozi za mara kwa mara kwa makocha wa timu mbalimbali za ligi hapa nchini ili kuweza kukuza soka hapa nchini.

Mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga Shadrack Nsajigwa amesema, katika ukuzaji wa soka hapa nchini inatakiwa watu sahihi na wenye uelewa mzuri wanatakiwa kutoa mafunzo kwa wachezaji ambao wataweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali hapa nchini na kuweza kuitangaza zaidi nchi.

Nsajigwa amesema, kozi nyingi na za mara kwa mara zinahitajika kwa ajili ya faida ya nchi ambapo itaweza pia kukuza vipaji vipya ili kuwaendeleza na hapo baadaye kuwa wanasoka wazuri zaidi na kuweza kuongeza vipaji vya soka hapa nchini.