Monday , 27th Jul , 2015

Uongozi wa timu ya Majimaji ya Mjini Songea umeanza mkakati kabambe wa kuhakikisha inafanya vizuri kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara msmu ujao ambapo imepanga kufanya ziara ya kimichezo nchini Malawi na Msumbiji.

Katika taarifa yake, Kocha wa timu hiyo Hassan Banyai amesema, wanatarajia kucheza michezo mitatu ya kirafiki wakati mitatu ikiwa ni ya hapa nchini na mingine miwili watacheza Malawi na Msumbiji.

Banyai amesema, katika michezo ya hapa nchini wanatarajia kucheza na JKT mlale, Tanzania Prisons na Mbeya City kwenye uwanja wa Majimaji Songea.

Banyai amesema, amepanga kusajili wachezaji 11 ambao watashirikiana na wachezaji waliokipandisha kikosi hicho wakati hadi sasa wakiwa wameshawasainisha wachezaji saba.