
Mwenyekiti wa mhama cha mpira wa pete Tanzania Anna Kibira amesema, vilabu sita kutoka bara ambavyo ni Uhamiaji Tanzania, Mbeya City Queens, JKT Mbweni, Jeshi Stars, Polisi Morogoro na Tumbaku Morogoro vitashiriki huku wakitakiwa kuhakiki ushiriki wao mapema.
Kibira amesema mpaka sasa kwa upande wa Zanzibar bado hawajamaliza ligi lakini watamaliza mapema ili kuweza kupata timu zitakazoshiriki Ligi ya muungano ambapo pia kutakuwa na vilabu sita shiriki huku mwisho wa uhakiki wa vilabu shiriki wa ligi hiyo ukiwa ni Novemba 20 ili kuweza kupanga ratiba.