Mjini Morogoro wakata miwa wa Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa maafande wa jeshi la Magereza nchini timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya, mchezo utakaopigwa katika dimba la Manungu Turiani.
Kwa upande wa mechi ya Yanga na Polisi Moro mechi hiyo imeahirishwa mpaka hapo itakapopangwa tena ili kuweza kuipa nafasi Yanga ambayo inayoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kuendelea kujiandaa na mchezo wa kwanza hatua ya 16 bora dhidi ya Etoile Du Sahel ya Tunisia mchezo utakaochewa Jumamosi wiki hii uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.