Akizungumza na East Africa Radio, Kharil amesema, timu yake inaundwa na vijana kutoka mikoa ya Morogoro, Arusha pamoja na Dar es salaam.
Kharil amesema, nchi shiriki za michuano hiyo, zinatarajia kuwasili mapema ili kuanza maandalizi ikiwa ni pamoja na kuzoea hali ya hewa pamoja na viwanja ili kuweza kuendana na mazingira ya kimchezo ambapo michuano hiyo inatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Anadir Burhan, Gymkhana na Chuo kikuu cha Dar es salaam. .
Michuano hiyo itashirikisha timu kutoka nchi za Namibia, Kenya, Uganda, Nigeria na wenyeji Tanzania ambapo zitashindana kwa muda wa wiki moja kupata mshindi wa michuano hiyo.