
Man City wakiwa katika basi na moja ya mataji yao
Klabu ya wanaume ya Man City ilikamilisha taji la tatu la ndani wikiendi iliyopita kwa kuifunga Watford jumla ya mabao 6-0 katika fainali ya kombe la FA, mataji mengine iliyoshinda ni la Ligi Kuu nchini Uingereza EPL na kombe la ligi 'EFL'. Timu ya wanawake ikishinda kombe la FA.
Katika video moja iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter, imemuonesha mshambuliaji wa klabu hiyo, Sergio Aguero akijilaumu baada ya kulidondosha taji la EPL kutoka juu ya basi walilokuwemo, lakini baadaye lilirudishwa tena.
Mapema jana Manchester City wakiwa kwenye parade ya kunogesha ubingwa wao, raha zikazidi mpaka la Premier League likandondoka bwana.@airtel_tanzania #AirtelMoneyBranch #TupoNaweKilaKona #ShabikiOS pic.twitter.com/AmkBDb4zwt
— SHABIKI on Saturday (@ShabikiOS) May 21, 2019
Sambamba na sherehe hiyo, Manchester City ilimtangaza kiungo, Bernardo Silva kuwa mchezaji bora wa msimu wa klabu hiyo kwa msimu wa 2017/18.