
Kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya Mtibwa Sugar Alhamis Agosti 24, 2018.
Kupitia taarifa yake, Yanga imethibitisha kuwa kama klabu haijatengeneza jezi mpya kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao hivyo bado wanatumia jezi zilezile za msimu uliopita katika mechi zao.
''Ifahamike kuwa bado hatujatangaza jezi mpya hivyo popote usikubali kununua jezi kwa kisingizio cha jezi mpya ya Yanga'', imeeleza taarifa.
Yanga imefafanua kuwa ipo kwenye mikakati ya kuhakikisha inakamilisha upatikanaji wa jezi mpya kwaajili ya mashindano yote msimu ya msimu huu ambapo itashiriki katika michuano mbalimbali ikiwemo ligi kuu na kombe la shirikisho nchini.
Yanga ilipitia changamoto ya kulazimika kutumia jezi zisizo na nembo ya mdhamini, kwenye mechi yao ya kwanza ya makundi kombe la shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger mwezi Mei mwaka huu.