Friday , 1st Jul , 2016

Mabeki wa Azam FC Shomari Kapombe na Serge Wawa wamewasili nchini baada ya kupata matibabu nchini Afrika Kusini.

Beki wa kati wa Azam FC, Serge Pascal Wawa

Kapombe ambaye alikuwa akisumbuliwa na tatizo la mfumo wa kusukuma damu anaendelea vizuri na anatarajia kuanza mazoezi.

Kwa upande wa Wawa raia wa Ivory Coast ambaye amekuwa akisumbuliwa na magoti, naye anatakiwa angalau kuwa na mapumziko ya muda wa zaidi ya mwezi mmoja.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema wana faraja kubwa kutokana na matibabu ya wachezaji hao kuwa na mafanikio.

Maganga amesema, wanaendelea vizuri kupitia matibabu hayo ya Afrika Kusini na sasa wanaendelea na tiba likiwemo hilo suala la Wawa kutakiwa kupumzika.