Tuesday , 24th Mar , 2015

Kocha wa Timu ya Taifa ya Soka la wanawake, Twiga Stars, Rogasian Kaijage amesema, mechi waliyoshinda nchini Zambia Shepopolo wanachukulia kama hakuna ushindi katika mechi hiyo ili kuweza kufanya vizuri zaidi katika mechi ya marudiano.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Kaijage amesema, katika mechi ya awali walicheza wakiamini ushindi upo upande wao kutokana na maandalizi mazuri japo wapinzani wao ni wazuri na wenye kucheza kwa ushirikiano.

Kaijage amesema, wanaamini mechi ya marudio ambayo itawapa picha ya kusonga mbele itakuwa ngumu kutokana na wapinzani wao Zambia kujiandaa kwa ajili ya kuweza kufanya vizuri ili kuweza kupata ushindi.

Twiga Stars ilianza vema kampeni yake ya kufuzu kwa fainali za michuano ya All African Games, itakayofanyika Congo Brazzaville baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 4-2 katika ardhi ya ugenini dhidi ya wenyeji Zambia huku marudio ya mchezo huo yakutarajiwa kurudiwa wiki mbili zijazo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.