Joe Hart
Hart alijiunga na klabu ya Torino ya nchini Italia kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu mwezi Agosti mwaka huu, baada ya kuambiwa kuwa alikuwa huru kuondoka na kocha wa Manchester City, Pep Guardiola.
Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 29, aliongeza kwa kusema kuwa aliona maamuzi ya Mhispania huyo, yanakuja kumwangusha.
"Kama hauendi kushinda, hakuna maana ya kupigana, hasa kwa mtu mwenye nguvu kama huyo". Alisema Hart.
Naye kocha wa City, Pep Guardiola, aliulizwa swali kuhusu mustakabali wa Hart, wakati akiongea na waandishi wa habari hii leo, amesema hakuna maamuzi yaliyofikiwa.
"Nimeshasema mara nyingi, kuwa mwishoni mwa msimu tutaona yupi mchezaji atakayecheka au kununa". Alisema kocha Pep na kuongeza " Yeye ni mchezaji wa Man City. Tutaamua mwishoni mwa msimu".


