
Afisa Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Crescentius Magori na msemaji Haji Manara.
Magori ameyasema hayo mapema leo kwenye mkutano na waandishi wa habari, ambapo ameeleza masuala mbalimbali ya klabu ikiwemo usajili wa wachezaji ambapo hadi sasa imebaki nafasi moja tu.
''Tungeweza kuunda kamati ya maadili lakini sheria ingesema mmemuundia kamati mzee Kilomoni, hivyo tusingeweza kuunda kamati kushughulikia kesi za nyuma'', amesema.
Aidha Magori ameweka wazi kuwa Bodi ya Wakurugenzi itaunda kamati ya maadili ambayo itashughulika na mambo yanayokuja huko mbele.
Kwa upande wa Mzee Kilomoni Magori amesema wamemfikisha mbele ya kamati ya maadili ya TFF, Kama mwanachama wa kawaida wa Simba na sio Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini kama anavyojieleza yeye.
''Mzee Kilomoni na wakili wake walishajulishwa kuwa hawana mamlaka na klabu tangu mwaka 2017 alipovuliwa uenyekiti wa Bodi ya Wadhamini hivyo anajua ila hataki kuelewa tu na hawezi kusumbua kama asilimia 99 ya wanachama wamekubali mabadiliko yeye asilimia 1 anatakiwa akubali tu hata kama hapendi''. ameeleza Magori.
Bodi ya wadhamini ya Simba kwasasa inaongozwa na Abdu Wahab Abbas, Ramesh Patel, Prof Juma Athumani Kapuya na Adam Iddi Mgoyi.