
Kharil amesema, amechagua vijana 14 ambao anaamini watatetea ubingwa wa michuano hiyo na ameangalia sehemu ambazo vijana wake walikuwa wakikosea ili kuhakikisha wanapambana na kuweza kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Septemba 11 mpaka 20 mwaka huu nchini kwa kushirikisha nchi za Nigeria, Soera Lione, Zambia, Botswana, Shelisheli, Msumbiji, Tanzania na wenyeji Afrika ya kusini.