
Francis Cheka mazoezini
Bondia Francis Cheka SMG wa Tanzania ambaye atashuka uliongoni Aprili 12 mwaka katika ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam kuvaana na bondia toka Iran hivi sasa amerejea jijini Dar es salaam na kuendelea na mazoezi mazito akijiwinda na mpambano huo wa kimataifa wa ngumi za kulipwa kuwania ubingwa dunia uzito wa Light Heavy kilo 81
Meneja wa bondia Francis Cheka Mohamed Abdalah 'Chief Kiumbe' amesema bondia wake yuko tayari na ana uhakika atailetea sifa Tanzania kwa kushinda mpambano huo na ndiyo maana yeye amekua akimpa sapoti ya kutosha katika maandalizi yake kwa kuwa anatambua siri ya ushindi katika mchezo wowote ni kufanya maandalizi mazuri na ya kutosha.
Kwa upande wao kocha wa bondia Francis Cheka Abdalah Salehe 'Komando' na Cheka mwenyewe wamesema wana uhakika wakushinda mpambano huo kwa kuwa wanafanya maandalizi ya nguvu ambayo walianza kwa muda mrefu tangu wakiwa Morogoro na baadaye Nairobi na sasa wamerejea hapa nchini wakiendelea na mazoezi mbalimbali wakijifua tayari kwa mpambano huo.
