
Rais wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare amesema, wameshampata kocha ambaye ni Mussa Benjamini Oyombi kutoka nchini Kenya na wameangalia ujuzi alionao katika kazi ya ngumi na wameridhika kuwa naye kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho.
Rwakatare amesema, wameshafanya mazungumzo na Oyombi na wamekubaliana na watamtumia kwani anauwezo wa kumpandisha bondia ulingoni kwa sheria za AIBA au shirikisho la Dunia la ngumi za ridhaa.
Rwakatare amesema, wanaamini kocha huyo kwa kushirikiana na makocha wengine wa Tanzania wataweza kuwapa mabondia mafundisho na njia mbalimbali katika mapambano.
Rwakatare amesema, kikosi kitaingia kambini kikiwa kamili mara baada ya mabondia wote ambao ni waajiriwa kupata ruhusa kutoka kwa waajiri wao.