Friday , 15th Jul , 2016

Tetesi nyingi za kuhusishwa kutaka kuihama Westham, pamoja na kiwango cha hali ya juu alichokionyesha kwenye michuano ya Mataifa ya Ulaya hivi karibuni, lakini hatimaye kiungo Dimitri Payet aibuka na kuvunja ukimya wa tetesi hizo.

Kiungo huyo wa klabu ya Westham, Dimitri Payet amesema hana mpango wa kuondoka kwenye klabu hiyo kwa msimu huu, baada ya kuwapo tetesi za kutakiwa na vilabu mbali mbali barani Ulaya.

Payet, aliyeng'ara na kikosi cha Ufaransa kwenye mashindano ya Mataifa ya Ulaya, yaliyomalizika hivi karibuni nchini mwao kwa kufunga mabao 3 katika mechi 7, ameelezwa kuwa ana thamani ya paundi milioni 100.

Mfaransa huyo amesema anaipenda klabu ya Westham, na hawezi kuwaambia mashabiki wa klabu hiyo neno la kuondoka.
…...........................