
Juma Kaseja
Akiwa ndani ya klabu yake ya KMC, Kaseja na wachezaji wenzake walipewa mapumziko ya siku tatu na kocha Jackson Mayanja, lakini Kaseja ameendelea na mazoezi kwa siku zote.
Akiwa katika mazoezi hayo ya peke yake Kaseja amesema, ''Mpira ndio maisha yangu na ili ucheze vizuri unahitaji mazoezi kwahiyo mimi sikuona kama nahitaji kupumzika nikaendelea na mazoezi ili kujiweka sawa''.
Akiongelea kuitwa Taifa Stars na kocha Ettiene Ndayiragije, Kaseja amesema amefurahi na yupo tayari kulitumikia taifa baada ya miaka 6 kupita bila kuitwa.
''Nafikiri ni wakati mzuri wa kutumikia taifa maana taifa kwanza mengine yanafuata, natamani tufike hatua ambazo mataifa mengine yanafika'', ameeleza.