Tuesday , 29th Dec , 2015

Timu ya Azam FC imesema imejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kuweza kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Afisa Habari wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema, Kocha Stewart Hall aliweza kugundua makosa yaliyojitokeza katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar na ameweza kuyafanyia marekebisho ili kikosi kuweza kufanya vizuri katika mchezo wa kesho.

Kwa upande mwingine Maganga amesema walikuwa na majeruhi wawili mlinda Mlango Aishi Manula na beki wa kati wa Klabu hiyo Aggrey Morris lakini kwa sasa Manula anaendelea vizuri na aliweza kucheza katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Kagera Sugar lakini Morris bado afya yake haijaimarika.

Maganga amesema, Morris aliumia katika maandalizi ya timu yake ya taifa ya Zanzibar Heroes wakati wakijiandaa kwa ajili ya michuano ya CECAFA ambapo hivi sasa ameshafanyiwa vipimo na anasubiri majibu ya daktari kujua kama atapata dawa au kufanyiwa upasuaji.