
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa kutokana na timu zote kutafuta pointi tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi ambapo Azam FC inashuka ikiwa inajivunia kuwa na pointi 32 ikishika nafasi ya pili ikipishana kwa pointi mbili na kinara Yanga yenye pointi 34 huku Mtibwa Sugar ikiwa na pointi 27 ikiwa nafasi ya tatu.
Mchezo mwingine wa kiporo utachezwa Januari mosi hapo mwakani kwa Ndanda FC kuwakaribisha Simba SC uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na baada ya hapo timu ya Azam FC, Yanga, Simba SC na Mtibwa Sugar zitaelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari tatu hapo mwakani.