Cheche amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari hii kuelekea mchezo wao wa raundi 29 ya ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Jumapili katika dimba la Azam Complex nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 1:00 usiku.
"Hali ya kikosi ipo vizuri kabisa na kila mtu anaonyesha ari ya kutaka kucheza wa mwanzo kwa hiyo tupo katika ushindani kwasababu tunategemea tushinde mechi hiyo ili tuweze kuongeza pointi zetu mbele. Majeruhi waliokuwepo kwenye kikosi ni wale ambapo yupo Yakubu pamoja na Daniel", amesema Cheche.
Pamoja na hayo, Cheche ameendelea kwa kusema "Kwa hiyo tunajipanga tofauti na vile tulivyojipanga mwanzo kwa sababu mwanzoni tulicheza uwanja tofauti na tulikuwa na baadhi ya wachezaji ambao sasa hivi hawapo, lakini sasa hivi tunajipanga kivingine kuhakikisha tunaendeleza ubabe wetu".
Mbali na hilo, Cheche amesema kwa sasa hawezi kuzungumza lolote kuelekea mechi yao ya mwisho dhidi ya Yanga kwa kuwa akili zao zote wamezielekezea katika mechi yao na Tanzania Prisons ila watahakikisha kila mechi wanapata ushindi.
Msikilize hapa chini Kocha Msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Idd Nassor Cheche akifunguka zaidi.