Friday , 2nd Feb , 2018

Kuelekea mchezo wa ligi kuu kesho kati ya wenyeji Azam FC dhidi ya Ndanda FC, kocha wa mabingwa hao wa Mapinduzi Aristica Cioaba amesema amewaandaa kiakili wachezaji wake kuhakikisha wanarejea kileleni kwenye mzunguko huu wa pili.

Kocha huyo raia wa Romania pamoja na kikosi chake kukabiliwa na majeruhi lakini watapambana kuhakikisha wanashinda mchezo huo kwasababu wachezaji amewaandaa vizuri kwa mchezo huo kiakili, kimwili na kila kitu.

“Nina wachezaji wawili majeruhi Wazir Junior ambaye ni mgonjwa huku Joseph Kimwaga akiwa bado anaendelea na mazoezi maalum kuelekea kurejea, mchezaji mwingine Sure Boy ana kadi nyekundu lakini Daniel Amoah huenda akarejea ila wachezaji wengine waliobaki wapo tayari kwaajili ya mechi'', amesema.

Kikosi hicho leo kitafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kukutana na timu hiyo kutoka mkoani Mtwara hapo kesho kwenye mchezo wa raundi ya 16 ya VPL. 

Azam FC na Ndanda FC zilicheza mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu huu na Azam kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye uwanja wa Nangwanda sijaona bao ambalo lilifungwa na mshambuliaji Yahaya Mohammed.