Katika taarifa yake, Afisa habari wa Azam FC Jaffar Maganga amesema, baada ya mechi hiyo dhidi ya JKT kikosi cha Azam FC kitacheza mchezo mwingine wa mwisho kabla ya msimu mpya wa ligi kuu ya Soka Tanznaia Bara kuanza.
Maganga amesema, Mchezo dhidi ya JKT Ruvu utakuwa ni kipimo cha ubora wa Timu hizo ambapo kocha wa Azam FC Stewart ataangalia wachezaji ambao wanaweza kumsaidia ikitokea wengine hawapo kama ilivyo sasa ambapo wengi wapo Timu ya Taifa.
