
Kocha wa Taifa Stars Emmanuel Amunike
Akiongea kwa mara ya kwanza tangu Stars ipoteze mchezo wake dhidi ya Senegal, Amunike ametaja vitu kadhaa vilivyopelekea kutokea kwa matokeo hayo ikiwemo ugeni wa wachezaji wake katika michuano hiyo.
''Kuna uoga mkubwa kwa wachezaji ambao tunajaribu kuuondoa kila siku na huwezi kuwalaumu ni mashindano yao ya kwanza, tunawajenga na wataendelea kuwa washindani'', amesema.
Kwa upande mwingine, Amunike ameongelea mchezo wa Stars unaofuata dhidi ya Kenya utakaopugwa Alhamis Juni 27, 2019, ambapo amesema kama ni hofu haitakuwepo kutokana na uhalisia kuwa Kenya ni timu ya jirani.
''Sidhani kama kutakuwa na ugeni kwenye mchezo dhidi ya Kenya, ni wenzetu wanaongea lugha moja na sisi, kikubwa ni hali ya kujiamini tu kwenye timu na wachezaji naamini wana kiwango kikubwa cha kuweza kupata matokeo'', ameeleza.
Kocha mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike akizungumza kuelekea mchezo wa pili wa AFCON dhidi ya Kenya utakaochezwa Alhamis Juni 27,2019 kwenye Uwanja wa 30 Juni Cairo pic.twitter.com/jszDsZ8zzh
— TFF TANZANIA (@Tanfootball) June 25, 2019