Tuesday , 1st Sep , 2015

Timu ya Taifa Stars inatarajia kuwasili nchini alfajiri ya kesho huku wachezaji wake Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngassa wakiwa wameshawasili nchini kwa ajili ya maandalizi ya mechi dhidi ya Nigeria Septemba 05 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa amesema, Stars iliyochini ya Kocha wake Boniface Mkwasa itaendelea na mazoezi hapo kesho jioni Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi ya wiki hii.

Mwesigwa amesema, kwa upande wa timu ya Nigeria mpaka sasa hajajua watawasili lini nchini lakini wameshawasiliana na Chama cha Soka nchini Nigeria NFF na wamethibitisha kuwasili nchini kabla ya mechi hiyo.