Ajibu kushoto na Chirwa kulia.
Ajibu ambaye yupo kwenye msimu wake wa pili ndani ya Yanga, leo amekuwa shujaa wa mchezo baada ya kufunga bao moja kusaidia bao moja hivyo kuhusika moja kwa moja kwenye mabao 2 kati ya matatu ya Yanga.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na Heritier Makambo dakika ya 18, Mrisho Ngassa dakika ya 25 kupitia pasi nzuri ya Ibrahim Ajibu ambaye naye alifunga la mwisho dakika ya 86 kwa shuti kali baada ya kupokea pasi kutoka kwa Deus Kaseke.
Ajibu sasa amefikisha mabao 3 msimu huu pamoja na msaada wa mabao 4, hivyo kuwa miongoni mwa wachezaji waliochangia mabao mengi ya Yanga katika mechi 8 ilizocheza mpaka sasa.
Katika hatua nyingine mchezaji wa zamani wa Yanga Obrey Chirwa leo ameonekana kwenye uwanja wa taifa akishuhudia mchezo huo. Chirwa aliondoka Yanga kenye usajili wa mwezi Julai na kujiunga na timu ya Nogoom El Mostakbal Football Club ya Ligi daraja la pili Misri.
Kuna tetesi kuwa huenda Straika huyo raia wa Zambia akarejea Jangwani kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Desemba.

