Saturday , 10th Feb , 2018

Kocha wa Yanga Mzambia George Lwandamina amemwanzisha nyota wa timu hiyo Ibrahim Ajib kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Barani Africa dhidi ya Saint Louis Suns United  leo jioni.

Katika kikosi kilichotolewa kwaajili ya mchezo huo Ajib ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa majeruhi siku za hivi karibuni lakini jana daktari wa timu hiyo Dr. Bavu alitoa ruhusa ya wachezaji hao kutumika kwasababu wamepona vizuri.

Mchezaji mwingine ambaye amepona na kuanzishwa kwenye kikosi cha leo ni kiungo Pius Buswita ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea Mbao FC na amekuwa akifanya vizuri ndani ya timu hiyo.

Moja ya vitu ambavyo vitaweka historia kwenye mchezo wa leo ni kuwepo kwa golikipa mwenye umri mdogo zaidi wa Yanga Ramadhani Kabwili akichukua nafasi ya Youthe Rostand ambaye ametoka kuumia na mwalimu kaendelea kumpumzisha licha ya kuwa amepona.

Saint Louis Suns United ambao ni mabingwa wa Shelisheli walitua nchini tangu Alhamisi tayari kwa mchezo huo wa hatua ya awali ya michuano hiyo mikubwa kwa vilabu Barani Afrika.

Kikosi Kamili

1. Kabwili 2. Kessy 3. Gadiel 4. Makapu 5. Yondani 6. Tshishimbi 7. Pius 8. Daud 9. Chirwa 10. Ajib  11. Martin

Akiba: Beno, Abdul, Nadir, Mahadhi, Mhilu, Mwashiuya.