
Mohamed Salah (10), akipongezwa na wachezaji wenzake wa Misri baada ya bao lake lililoivusha timu robo fainali za AFCON
Mshambuliaji wa AS Roma, ya Italia, Mohammed Salah, aliifungia Misri, bao pekee kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni, kunako dakika ya 11, baada ya kuupitisha vizuri mpira kwenye ukuta wa wachezaji wa Ghana.
Nayo Mali iliungana na Uganda, kufunga safari ya kurejea kwao, baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo.
Uganda, iliyokuwa inawakilisha ukanda wa Afrika Mashariki, imemaliza nafasi ya nne ikiwa na pointi 1, pekee baada ya kufungwa mechi mbili na kutoka sare mechi moja.
Michezo ya robo fainali, za AFCON, itaendelea kutimua nyasi, mwishoni mwa wiki hii, pale Burkina Faso ikipepetana na Tunisia saa moja kamili usiku, wakati, Senegal ikioneshana kazi na Cameroon saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Nayo DR Congo itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Ghana saa moja kamili usiku, wakati saa nne za usiku Misri itaoneshana ubabe na Waarabu wenzao wa Morocco.