Wednesday , 18th Nov , 2015

Msanii na Producer Cjamoker ambaye ameachia wimbo wake wa Sijaona, amesema muziki wa sasa hivi watu wengi wana uelewa nao, hivyo inakuwa changamoto kubwa kwao wasanii.

Cjamoker ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kuwa watu wengi sasa hivi wanatoa maoni yao juu ya muziki, na iwapo unaharibu watakudharau.

“Muziki wa Bongo sasa hivi watu wanaelewa muziki mzuri, wanasema na wanashauri, ukianza kuleta kwele wanakutupia mawe, ni changamoto sana”, alisema Cjamoker.

Pia Cjamoker ameongelea wimbo wake mpya ambao ameuimba na sio kurap kama alivyozoeleka na kusema kuwa amefanya hivyo kwakuwa anataka kuonesha jamii kwamba hata kwenye kuimba anaweza kufanya vizuri.

“Nimeamua kuimba kwenye wimbo huu badala ya kurap kwa sababu siku hiyo niliamka na vibe ya kuimba, unajua hata rafiki zangu wamenikariri kuwa mimi ni mwana Hip Hop sana, ila mi kokote nasimama kama hivi nilivyofanya kwenye Sijaona”, alisema Cjamoker.

Cjamoker ameulezea wimbo huo ambao ameuachia siku tatu zilizopita na kusema kwamba ni wimbo unahusu mapenzi.