
Nikki wa Pili akiwa na Kala Jeremiah
Hayo yamebainishwa na rapa Nikki wa Pili pamoja na Kala Jeremiah walipokuwa wanazungumza na www.eatv.tv katika nyakati tofauti tofauti, na kuwashukuru mashabiki zao kwa kuweza kuwapendekeza kuwa viongozi kupitia kipindi cha FUNGUKA kinachorushwa katika ukurasa wa Facebook wa EATV pamoja na runinga.
"Nafikiri huo ni mtazamo wao na wanaona labda inaweza ikawa ngazi ya ku-build kuelekea ile ndoto yangu ya Urais. Kwa hiyo mimi naheshimu mawazo yao lakini kwa upande wangu ni jambo ambalo sijawahi kufikiria ila naheshimu mawazo yao", amesema Nikki wa Pili.
Pamoja na hayo, Nikki wa Pili ameendelea kwa kusema kuwa "kiukweli hayo ni mawazo yao na mimi nayaheshimu na katika maeneo ambayo sikuwahi kuyafanyia maamuzi ni juu ya kujiunga na chama chochote cha siasa, hivyo kama wao wamenichagulia CCM basi itakuwa ni mtazamo wao tu lakini kwangu ndio kitu kinachonisumbua kukipatia maamuzi kwa kipindi kirefu".
Kwa upande wake, rapa Kala Jeremiah amesema hakuwahi kufikiria kujiingiza katika masuala ya kisiasa, na kudai baada ya kuwepo kauli nyingi kutoka kwa watu wanaomzunguka amejikuta akitamani kujikita kwenye masuala ya kisiasa.
"Ni jambo zuri sana kwa wananchi kunipendekeza maana kwangu mimi nalichukulia jambo hilo kama baraka kwangu, kwa kugundua kipaji cha uongozi maana hata zamani viongozi walikuwa wakipatikana kutumia njia hiyo.....Nitakapoingia kwenye siasa sitogombea Ubunge kwa sababu mimi ninaamini nimeshawawakilisha wananchi katika 'level' za juu sana tokea zamani kupitia muziki wangu....
Kitakachokuwa kimenivuta hasa mimi kuingia katika siasa ni kugombea nafasi ya Urais kwa kuwa hiyo ndio ndoto yangu kubwa, na nikiwa Rais ndio nitaleta mapinduzi wanayoyataka wananchi", amesema Kala Jeremiah.
Kwa upande mwingine, Kala Jeremiah amesema suala la kugombea urais kwake ni jambo dogo, kwa kuwa hadi dakika hii anazo sera zinazomuwezesha kuwatumikia wananchi ambazo alishawahi kuziimba katika wimbo wake wa 'ningekuwa rais' huku akidai kama ni mapungufu ya sera hiyo ni machache ya kuongezea tu ila mengi bado yapo hai hadi leo hii.