Friday , 28th Feb , 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi leo hii ameitisha mkutano wa wasanii na waandishi wa habari kuhamasisha wasanii kutambulika kikatiba na pia kuingizwa kwa sheria ya hakimiliki ya kazi za wasanii katika Katiba mpya pamoja na kuzindua kampeni ya kitaifa kuimiza wasanii kutambulika kikatiba..pamoja na haki bunifu pia.

Mkutano huu pia umehudhuriwa na Professa Jay, Dani Msimamo, G Nacko, Joh Makini, Producer P Funk, Komando Hamza kalala kati ya wasanii wengine ambao kwa pamoja wameungana katika jitihada za kuleta mabadiliko na kutetea maslahi ya wasanii ili kuwawezesha kufaidika na kazi zao za sanaa katika siku za usoni.

Nikki ameongea nasi kuhusiana na tukio hili ambapo Nicki amesema kuwa huu ni uzinduzi rasmi wa kampeni ya kutetea haki za wasanii ambapo ameomba mashabiki kuwaunga mkono katika harakati hizi.