
Master Jay ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa iwapo msanii ana uwezo wa kuwa na timu, basi ni muhimu kuwa na timu ambayo itamuweka katika muonekano mzuri pia.
“Unajua kama msanii ukishafika levo flan kwenye jamii au soko lote, kwenye macho ya watu umekuwa kama brand tuseme, unavyokuwa kwenye video unaonekana kama star, kwa hiyo ni lazima uwe na timu ya kispecialist ambayo ndio inakushauri”, alisema Master jay.
Master Jay aliendelea kusema kuwa kwa siku za nyuma ilikuwa ngumu kutokana na soko la muziki wa Tanzania lilikuwa halijapanuka, kama ilivyo sasa hivi, ambapo wasanii wanaingiza pesa nyingi kutokana na soko la muziki kukua.
“Lakini mi naona tutafika kwa sababu soko letu letu lilikuwa ni dogo hela ilikuwa ni ndogo, sasa hivi wasanii wanatengeneza hela nyingi, the more money they have inamanisha wanaweza wakawa na timu, kuna wengine wameshakuwa na timu, ana management, ana DJ, ana Stylist”, alisema Master Jay ambaye ni moja ya watayarishaji muziki wenye heshima kubwa kwenye Bongo Fleva.