Wahu amesisitiza kuwa, ameweka familia yake mbele kwasababu kwake linapokuja swala la malezi ya watoto, haijalishi muziki unalipa kiasi gani, haipo sahihi kulipa mtu mwingine kufanya kazi hii ka niaba yake.
Hata hivyo, kauli hii ya Wahu haimaanishi kuwa ameweka kando muziki, na maelezo haya ameyatoa baada ya kushuka jukwaani kutumbuiza katika onyesho huko Ngara, akionyesha kuwa ana mpango maalum wa kuhakikisha kuwa anasongesha vitu hivi viwili katika mpangilio.