Tuesday , 14th Feb , 2017

Msanii wa bongo fleva Mb Dogg amesema muziki ni kama upepo na kipindi hiki upepo huo wa muziki haupo upande wake hivyo mashabiki zake wamuelewe.

Mb Dogg

 

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Mb Dogg amesema muziki ni kama maisha kuna kipindi cha kupanda na kushukma na kwamba kipindi hiki upepo haupo wakati wake hivyo mashabiki zake wanapaswa kumuelewa na kutambua kwamba kwa sasa upepo upo upande wa pili.

Hata hivyo Dogg amesema kuna mipango ambayo anaipanga kwa sasa na menejimenti yake na mambo yakikaa sawa atarudi kwenye 'game' kwa kuwa sasa kuna simu nyingi zinamuhamasisha kurudi kwenye muziki.