Friday , 14th Mar , 2014

Msanii MB Dogg, ambaye baada ya ukimya wa muda mrefu akiwa anafanya mambo mengine ikiwepo suala zima la kuigiza filamu, ameamua kurejea katika sanaa ya muziki na ngoma mpya inayokwenda kwa jina 'Umenuna'.

MB Dogg ameweka wazi kuwa, kukaa nje ya muziki kiukweli kumezua hisia tofauti kutoka kwa mashabiki na wadau mbali mbali wa muziki, wakiwepo wale waliodai kuwa kaishiwa, na hapa anafunguka mwenyewe juu ya hali halisi ilivyokuwa.