Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, kura zinazopigwa na mashabiki ndani ya mwezi huu mzima zinachangia asilimia 70 ya maamuzi ya nani atakayeibuka mshindi, na asilimia 30 itakayobaki itaamuliwa na timu ya majaji iliyoteuliwa kuendesha zoezi hilo.
Kupiga kura kwa mshiriki ambaye unampenda ashinde tuzo, kwa njia ya sms andika namba ya mshiriki unayempenda na utume kwenda namba 15440 ama piga kura kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya https://www.kililager.com/ktma.