Monday , 14th Apr , 2014

Kundi maarufu la maigizo la nchini Uganda, The Ebonies wamefanikiwa kuzindua mchezo wao mpya wa maigizo ambao unakwenda kwa jina ‘Amaanyi g’omuhabati, kwa tafsiri ya Kiswahili nguvu ya upendo, mchezo ambao unabeba mafundisho mengi ya kifamilia.

The Ebonies

Watatibu wa shughuli hii iliyofanyika kwa mafanikio makubwa wameweka wazi kuwa, umuhimu wa michezo kama hii ya maigizo unatokana na uwezo mkubwa wa sanaa hii kufikisha ujumbe fulani na kubadilisha jamii, kama vile ilivyo sanaa ya muziki.

Tukio la uzinduzi wa mchezo huu, ambalo lilipambwa na burudani mbali mbali za muziki pamoja na sarakasi, pia lilihudhuriwa na wageni mbalimbali wazito, akiwepo makamu wa rais w Uganda, Mheshimiwa Edward Ssekandi.