tamasha la muziki la Karibu Music nchini Tanzania
Wasanii mbalimbali wakiwemo Prof, Jay, Barnaba Boy, Juma Nature na wengineo wengi wamepanga kuimba nyimbo zao mbalimbali na pia kuonesha aina ya muziki wa Live na wa asili kwa kutoa burudani kuanzia kwa watoto mpaka watu wazima.
Tamasha hili linafanyika kwa siku Tatu mfululizo kuanzia leo mpaka Jumapili likiambatanisha Burudani ya muziki na semina juu ya sanaa hii kwa washiriki.