Wednesday , 12th Mar , 2014

Mwisho wa wiki hii umekuwa si shwari kwa Mtayarishaji wa Muziki kutoka Seductive Records, Mr T Touch ambaye ndiye mpishi wa ngoma kali kama vile Kimugina ya Linex na Nakula Ujana ya Ney kati ya nyinginezo.

Hivi sasa Mr T-Touch anauguza majeraha baada ya kupata ajali mbaya ya Bajaji ambayo nusura ichukue maisha yake, akiumia katika maeneo ya bega na kichwani wakati akiwa anatoka Coco Beach.

Mr T-Touch ameiambia enewz kuwa alikuwa amepanda Bajaj pamoja na Msanii wake mmoja anayefahamika kwa jina Bija, na tukio hili baya lilisababishwa na mwendokasi wa dereva huyo wa bajaj.