Msanii wa miondoko ya bongofleva Staric Richard
Mkali huyo anayekuja juu katika tasnia ya muziki ametoa ya moyoni akimtaka Rais Magufuli kuendelea kuwapa kipaumbele wasanii wa muziki wapate haki zao na pia kutambulika na kuheshimika.
Staric ambae asili yake ni Msukuma kutoka Mwanza ameongezea kuwa pamoja na pongezi hizo za rais, hivi sasa ametoa kazi yake mpya ikiwa ni kichupa kipya kabisa alichokibatiza jina 'Kata' wimbo ambao ameufanyia kupitia lebo ya freenation chini ya prodyuza T-Touch na kuongozwa na Tonee Blaze.