Monday , 16th Nov , 2015

Nyota wa muziki Size 8 wa Kenya pamoja na mumewe DJ Mo, wameweka bayana jinsia ya mtoto wao wa kwanza kuwa atakuwa ni wa kike, habari ambazo wamezidhihirisha katika sherehe ya maandalizi ya mapokezi ya mtoto waliyoifanya mwishoni mwa wiki.

Nyota wa muziki Size 8 wa Kenya

Sambamba na kuweka wazi jinsia ya mtoto wao, Mastaa hawa pia wamepata wakati mzuri wa kusherekea pamoja na watu wengine mashuhuri, marafiki wa karibu na familia katika maandalizi ya ujio wa binti yao huyo katika sherehe iliyonakshiwa katika maudhui ya rangi nyeupe na pinki.

Size 8 anajitengenezea heshima ya aina yake pia kwa kuwa funzo kwa wanawake wengi ambao bado hawajapitia ujauzito, kutokana na kuwa mstari wa mbele kuweka bayana uzoefu anaopitia katika kipindi chote cha ujauzito wake kuelekea kuwa mama.